Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, almeoa matamshi hayo leo Jumatatu baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kufanya mashambulizi yasiyopunguua 20 ya anga dhidi ya maeneo kadhaa muhimu katika mkoa wa al-Hudaydah magharibi mwa Yemen, ikiwa ni pamoja na kituo cha umeme cha Ras al-Khatib katika jimbo hilo.
Mashambulizi hayo, amesema, ni mwendelezo wa uchokozi wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya maeneo muhimu ya kiuchumi ya raia katika eneo la Peninsula ya Arabia kama bandari, viwanja vya ndege, na vifaa vya kuhifadhia chakula.
Ameutaka Umoja wa Mataifa ukomeshwe utepetevu wake katika kukabiliana na ukatili uliokithiri unaofanywa na utawala huo kwa uungaji mkono wa kisiasa na wa pande zote wa Marekani na nchi kadhaa za Magharibi.
Baqaei ameongeza kuwa msaada na uungaji mkono huo vimeufanya utawala huo kuhisi kuwa na uhakika wa kutoadhibiwa, licha ya uhalifu wake mbaya katika eneo la Asia Magharibi.
Ametaja vita vya mauaji ya kimbari vya Israel vinavyoendelea tangu Oktoba 2023 dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na kesi nyingine za mauaji ya kimbari katika maeneo yote yanayokaliwa kwa mabavu kuwa ni mfano hai wa ukweli huo.
Katika muktadha huo huo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani ukiukaji wa mapatano wa kusitisha vita unaoendelea kufanywa na utawala wa Israel dhidi ya Lebanon.
342/
Your Comment